USAFI
- depatrick2020
- Feb 12, 2022
- 1 min read
Vijana washarika wa KKKT Tunduma wakiendelea na kampeni yao ya usafi wa mazingira yazungukayo usharika huo.
Kwenye picha ni baadhi ya vijana kutoka vijiji na mitaa mbalimbali ndani ya usharika wa Tunduma wakiendelea na kazi.
Kampeni hii imekuwa endelevu toka ilipoanzishwa mwaka 2021 hata sasa imekuwa yenye kuzaa matunda na mafaniko mengi yameonekana siku hata siku.

Baada ya kufanya mahojiano na baadhi ya washiriki wa kampeni hii wengi walionyeshwa kufurahishwa sana na namna ambavyo wamezidi kupata fursa ya kufahamiana zaidi na vijana wenzao pia hata kupata wasaa mzuri wa kubadilishana mawazo.
"Nafurahi sana kushiriki katika tendo hili kwasababu kwangu linanipa amani kuwa kijana mwenye nguvu ambaye natumia nguvu zangu kuwezesha na kupendezesha mazingira yangu ya kuabudia" Alisema mmoja wa vijana hao kutoka kijiji cha Maporomoko.
Kampeni hii hufanyika kila Jumamosi za mwisho wa mwezi na ni mwanzo mzuri kabisa hata imekuwa ni mfano wa kuigwa kutoka kwa vijana wa sharika nyingine ndani na nje ya jimbo la Magharibi.

Vijana wakijipongeza kwa vinywaji baridi baada ya kazi nzito siku ya Jumamosi tr 12-02-2022
Tafadhari endelea kutufuatilia katika mitandao yetu ya kijamii Facebook, Instagram na Youtube channel yetu ya UV-KKKT TUNDUMA TV ili kufahamu mengi zaidi.
Kommentare