
EDGAR PATRICK
7 May 2021
Mrejesho kwa safari ya kwenda kuwatembelea wahitaji
Bwana wetu Yesu kristo asifiwe!!
Tunapenda kuwashukuru sana wote walihusika katika kufanikisha safari yetu ya kwenda kuwaona wahitaji na wagonjwa mahospitalini siku ya tarehe 08-05-2021, MUngu azidi kuwabariki na kuwazidishia maisha mema zaidi, amen.
Ufuatao ni mrejesho wa namna safari hii nzima ilivyofanyika kuanzia mwanzo hata ukamilikaji wake, Tafadhari ungana nami ripota wako nikujuze.
Baada ya kupata wazo hili tulianzisha michango kutoka kwenu vijana na washarika wa usharika wetu KKKT Tunduma ambapo tulifanikiwa kupata kiasi cha 370,000Tsh pamoja na debe 4 na medaa 3 za mchele,sabuni za kuogea,na za mche dazani 2,sabuni za unga pakti 5 pamoja na ndoo moja katoni mbili za juice ya embe, nguo na viatu.
Kutoka kwenye pesa hiyo 370,000Tsh tulinunua chumvi, sabuni, juice, sukari, biskuti,nk
Tulianza kwanza kabisa kwa kuwatembelea watoto yatima katika kituo cha malezi MBOZI MISSION ambapo tulishiriki kwa kupiga nao picha kufurahi nao pamoja kwa michezo nyimbo na mambo mengine mengi.
Baada ya hapo tulisonga zaidi na kufika katika hospitali ya mkoa Vwawa ambapo tulitembelea wodi za kina mama na wagonjwa mahututi na kufanya maongezi na dakri wa zamu wa siku hiyo hata kushiriki nae kwa picha ya pamoja, mwisho tulimalizia kwa kuwatembelea watoto yatima katika kituo cha upendo hapa Tunduma ambapo nao turishiriki nao kwa matukio mbalimbali na ratiba yao ya siku hiyo.
MUNGU azidi kuwabariki tena na tena na ninakusihi kijana mwenzangu usiwahi choka kusaidiwa wahitaji kwani kupitia wao tunapata thawabu za Mwenyezi MUNGU,
Nikutakie wakati mwema zaidi ni mimi ripota wako kutoka UV-KKKT TUNDUMA TV
EDGAR PATRICK


