
EDGAR PATICK
9 Sept 2021
Msiba wa aliyekuwa kiongozi wa Idara ya michezo ndugu Idan Nzikalila
Uongozi wa umoja wa vijana KKKT Tunduma kwa masikitiko makubwa mno wanatangaza msiba wa aliyekuwa mwenyekiti wa idara ya michezo IDAN NZIKALILA ambae amepatwa na mauti akiwa njiani kuelekea kupata matibabu baada ya kuugua kwa muda.
Uongozi unawapa pole wote walioguswa namna moja ama nyingine wana familia ndugu jamaa na marafiki wa kaka yetu mpendwa Idani, pia pole kwa wana umoja wote na haswa viongozi kwa kupungukiwa na nguvu kazi katika idara husika.
Ratiba za mazishi zimepangwa na familia yenyewe yaani wazazi wa marehemu amabapo msiba umepangwa kufanyika nyumbani kwa wazazi wa marehemu mjini Mafinga mkoani Iringa.
Hivyo tunawatangazia vijana wote wa usharika wa Tunduma na wale wote wanaohusika kuwa Umoja wa vijana umepanga safari ya kwenda msibani kushiriki mazishi ya kumwuaga marehemu safari itakayo anza mapema kesho tarehe 11-09-2021 asubuhi saa 12:00 tukiondoka na basi la pamoja, sambamba la hilo tumeanzisha kampeni fupi na kupata michango ya rambirambi kwa kila kijana aliyeguswa, kiasi cha mchango huu ni kuanzia Tsh2,000 au zaidi kwa mtu mmoja.
Tafadhari kwa wewe utakaye ungana na waombolezaji kusafiri unaombwa kuwasirisha mapema mchango wako wa rambi rambi jina pamoja na nauli kwa viongozi wako.
"BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE MILEE!, AMINA"


