top of page
  • Facebook
  • YouTube
  • Instagram

MKESHA WA KUFUNGA MWAKA 2021

EDGAR PATRICK

31 Dec 2021

Baada ya kukaa chini na kutafakari ukuu wa Mungu juu ya mambo ambayo vijana wametendewa kwa mwaka 2021viongozi na wana umoja wenyewe walikubaliana kuweka mkesha wa shukrani na maombezi kwa wahitaji.

Mkesha ambao ulifanyika usiku wa tarehe ya 31 ya mwezi wa 12 mwaka uliopita, sambamba na maono hayo iliundwa timu maalumu ya kusifu na kuabudu kutoka vijana wa umoja huo,

Walialikuwa kwaya mbalimbali kutoka kwenye makanisa jirani ili waje kuungana na vijana wenzao katika tukio hili maalum, ambapo mchungaji wa usharika huo wa Tunduma Mhungaji kiongozi EZEKIEL MWANDUGHULILE alifunguka mkesha huo kwa neno na baadae kwaya mbali mbali na timu za kusifu na kuabudu kutoka makanisa mbali mbali walishiriki kwa kusifu na kuabudu kuimba na kucheza kwa furaha.


Mwenyekiti wa umoja huo BW. EMMANUEL MWATWEBE ambaye pia ndie mwasisi na msimamizi wa UMOJA WA VIJANA USHARIKA WA TUNDUMA akizungumza na wanahabari alisema kwamba binafsi anamshukuru MUNGU kwa namna ambavyo amezidi kumbariki yeye na familia yake lakini pia kumpatia maono ambayo yamezidi kuchipua matunda kadri muda unavyozidi kwenda na hata kwa sasa wao kama viongozi wana mipango mingine mingi zaidi ya kuzidi kuwaandaa na kuwakutanisha vijana pamoja katika michezo, ibada, mikesha na matukio mbali mbali ili kuzidi kufahamiana zaidi na kujengana kiroho kimwili na hata kiuchumi.


Akiongezea kusema kwamba wameanza na ufunguzi wa kikundi katika mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook Intagram, Whatsapp na sehemu zingine pekuzi ili kuzidi kuwafikia na kuwaita vijana wengi zaidi kushuhudia kile kinafanywa na wenzao kwa maana ya kuzidi kusafirisha injili ya kristo,pia alisema kuwa wameweza kufungua kikundi cha kimtandao cha utunzaji fedha (M-KOBA) ili kurahishisha ufikishwaji wa michango hata kwa wale walio mbali na mji wa Tunduma.


BW. Emmanuel mwatwebe alimalizia kwa kuwakaribisha vijana wa usharikawa Tunduma na hata wale wa maeneo mengine kuzidi kuungana na kushirikiana ili kuifanya kazi ya MUNGU kwani vijana ndio nguvu kazi ya kanisa.


Imeandaliwa na mimi

EDGAR PATRICK

Abstract Linear Background

Find Us On

Follow Us on Instagram:

  • Facebook
  • YouTube
  • Instagram
  • Whatsapp

@uv_kkkt_tunduma

@2022

proudly created by Edgar Patrick

SHERIA

Tel: +255 656 746 107

+255 628 724 476

Email:Officialuvtunduma@gmail.com

FAQ
bottom of page